Ule mpambano uliokuwa ukisubiriwa kwa hamu na wapenzi wa soka nchini, kati ya kikosi cha wana Jangwani, Young African na Al ahly ya Misri uliochezwa leo uwanja wa Taifa, hatimaye umemalizika kwa Yanga kuifunga goli 1 Al ahly kupitia mchezaji mahiri Nadir Haroub ‘Canavaro’ mnamo dakika ya 82 kipindi cha pili na kuifanya Yanga kuondoka na pointi 3 muhimu.
BAO
pekee la Nahodha Nadir Haroub Ali ‘Cannavaro’ jioni hii limeipa ushindi
wa 1-0 Yanga SC katika mchezo wa kwanza wa kuwania kucheza Hatua ya 16
Bora Ligi ya Mabingwa Afrika, dhidi ya Al Ahly ya Misri Uwanja wa Taifa,
Dar es Salaam.
Cannavaro alifunga bao hilo dakika ya 87 akimalizia kona maridadi ya winga Simon Msuva kutoka wingi ya kulia.
Kona hiyo ilitokana na kipa Sherif Ekram Ahmed kupangua shuti kali la mshambuliaji Mganda, Emmanuel Okwi.
Katika
mchezo huo uliochezeshwa na refa Heileyesus Bazeze aliyesaidiwa na
Kindie Mussie Tdedesse Shawangiza wote kutoka Ethiopia, hadi mapumziko
milango ilikuwa migumu.Shujaa; Beki Nadir Haroub 'Cannavaro' akipongezwa na wenzake Emmanuel Okwi na SImon Msuva baada ya kufunga bao pekee jioni dhidi ya Al Ahly |
Yanga SC ndiyo waliotawala zaidi mchezo na kutengeneza nafasi kadhaa nzuri za kufunga, lakini wakakosa umakini katika kumalizia.
Simon
Msuva alikuwa chanzo kizuri cha mashambulizi ya Yanga upande wa kulia,
lakini Waganda Emannuel Okwi na Hamisi Kiiza walishindwa kutumia nafasi.
Haruna Niyonzima, Frank Domayo na Mrisho Ngassa kwa pamoja walicheza vizuri katika safu ya kiungo kipindi cha kwanza.
Kipindi
cha pili, Ahly kidogo walibadilika na kuongeza kasi ya mashambulizi
kupitia kwa Amr Gamal, ambaye hata hivyo alidhibitiwa vikali na walinzi
wa Yanga, ambao leo walicheza kwa umakini wa hali ya juu.
Mabadiliko
yaliyofanywa na kocha Mholanzi Hans van der Pluijm, kumuingiza
mshambuliaji Didier Kavumbangu kuchukua nafasi ya Hamisi Kiiza yalifufua
makali ya safu ya ushambuliaji ya timu hiyo.
Winga wa Yanga SC, Simon Msuva kushoto akimtoka beki wa Al Ahly
.
Mshambuliaji wa Yanga SC, Emmanuel Okwi akiwatoka mabeki wa Ahly |
Kavumbangu
aliwapa wakati mgumu mno mabeki wa Ahly tangu alipoingia dakika ya 66
hata mashabiki wa Yanga wakatamani angekuwa uwanjani tangu mwanzo.
Pamoja
na kufungwa 1-0, Al Ahly inayofundishwa na kocha Mohamed Yousef,
ilionyesha upinzani kwa Yanga SC, jambo ambalo linaashiria katika mchezo
wa marudiano lolote linaweza kutokea.
Baada ya matokeo haya, Yanga SC sasa inahitaji sare ya ugenini ili kusonga mbele hatua ya 16 Bora.
Kihistoria
hii inakuwa mara ya kwanza kabisa Yanga SC inapata ushindi dhidi ya
timu ya Misri na Kaskazini mwa Afrika kwa ujumla, kwani mara zote
imekuwa ikifungwa na kutoa sare.
Kikosi
cha Yanga SC leo kilikuwa; Deo Munishi ‘Dida’, Mbuyu Twite, Oscar
Joshua, Nadir Haroub ‘Cannavaro’, Kevin Yondan, Frank Domayo, Simon
Msuva, Haruna Niyonzima, Hamisi Kiiza/Didier Kavumbangu dk66, Emmanuel
Okwi na Mrisho Ngassa/Said Bahanuzi dk87.
Al
Ahly; Sherif Ekramy Ahmed, Saad El-Din Saad, Mohamed Ghareeb, Ahmed El
Moneim, Sayed Abdel Waheed, Shihab Eldin Saad, Hossam Mohammed, Ramy
Abdel Aziz, Moussa Yedan/Mahmoud Ibrahim dk59, Mohamed Ismail/Ahmed
Shakri Abdelraouf dk 73 na Amri Gamal Sayed/Ahmed Raoud Adam dk88.
0 comments:
Post a Comment