Msemaji kampuni ya Weusi, Nick wa Pili amesema kuwa rapper Lord Eyez amesimamishwa na kampuni hiyo kutokana na kuvunja maadili.
Nick
wa Pili amesema baada ya kupokea taarifa za Lord Eyez kushikiliwa na
polisi huko Arusha kwa wizi wa Laptop walikaa kikao na kuamua
kumsimamisha.
“Kitu ambacho naweza kusema kutoka Weusi ni kwamba Lord Eyez tumemsimamisha kazi kikampuni,”
“Uamuzi wa kumsimamisha tumeufikia jana na leo ndio tumeamua kutangaza rasmi kwamba Lord Eyez tumemsimamisha kazi na amesimamishwa kutokana na misingi na makubaliano ya kampuni,kulingana na maadili ya kampuni yetu na mawazo yetu kwa pamoja ndio yamefanya tukamsimamisha. Kwahiyo ni kwamba tumemsimamisha kutokana na makubaliano ambayo yalifikiwa ndani ya kampuni ambayo mengine yatabakia ndani ya kampuni.” Nikki wa Pili

Uamuzi
huo wa Weusi umekuja kufuatia taarifa kuwa Lord Eyez alikamatwa na
polisi kwa tuhuma za wizi wa laptop Jumamosi, huko Arusha na baadhi ya
picha za tukio hilo kuonekana. Taarifa hizo zimedai kuwa anatuhumiwa kwa
wizi wa laptop aina ya ‘Dell’.
Mwaka
juzi, Lord Eyez alikamatwa na kufikishwa mahakamani kwa tuhuma za wizi
wa Power Window za gari la Ommy Dimpoz, lakini Ommy alitangaza kumsamehe
msanii huyo.
0 comments:
Post a Comment