Wednesday, March 5, 2014

12:14 AM


Ni muda mfupi tu toka Uganda ipitishe sheria ya kupinga ushoga, imeripotiwa mtu mmoja aliyetuhumiwa kuwa shoga alichomwa moto mpaka kufa nchini humo.
CNN imeripoti tukio hilo ambalo jina la mtu  huyo halikuweza kujulikana. Picha ilionesha jinsi mtu huyo anavyochomwa moto huku akiwa pembeni mwa reli huku watoto wakishuhudia tukio hilo.
Sheria hiyo iliyopitishwa hivi karibuni, inahusisha pamoja na kufungwa maisha kwa mtu yoyote atakayejihusisha na shughuli zozote za ushoga pamoja na kuambukiza ukimwi, matendo ya ngono na watoto pamoja na watu wenye ulemavu, udhalilishaji ikiwa ni pamoja na ubakaji.
Sheria hiyo iliyozaliwa mwaka 2009, na kupewa jina “Kill The Gays” ikimaanisha “Ua Mashoga” ambayo ilisisitiza hukumu ya kifo kwa matendo fulani ya ushoga, lakini ilirudishwa kabatini kutokana na kelele nyingi zilizopigwa na mataifa mbalimbali.


0 comments:

Post a Comment