Amiri Jeshi Mkuu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.
Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akipewa maelezo kwa kutumia mchoro kuonesha
mzunguko mzima wa maeneo atakayotembelea katika kikosi cha Komando
ARIDHISHWA NA UTIMAMU WA VIKOSI HIVYO
- AAHIDI TATIZO LA MAJI KUPATIWA UFUMBUZI NDANI YA MWAKA 2014
- KIKOSI CHA UHANDISI WA MEDANI CHAAHIDIWA VIFAA ZAIDI ILI KUPAMBANA NA MAJANGA NCHINI
- AAGIZA JWTZ KUBUNI MIKAKATI YA KUONDOKANA NA MAKAZI YA MUDA
Ziara hiyo ya siku moja ilihudhuriwa pia na Mkuu wa Mkoa wa
Morogoro Mhe. Joel Bendera, Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue,
Wakuu wa Kamandi, Wakuu wa Matawi Makao Makuu ya Jeshi, Makamishna
Wizarani na Wajumbe wa Mabaraza ya Ulinzi na Usalama wa Wilaya na Mkoa
wa Morogoro.
(Na Luteni Kanali Juma Nkangaa Sipe, Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Wizara ya Ulinzi na JKT)
Amiri Jeshi Mkuu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe.
Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akiwasili kwenye Kikosi cha Komando kuanza
ziara yake ya kujionea hali na utimamu wa vikosi vya JWTZ Mkoani
Morogoro.
Amiri Jeshi Mkuu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.
Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akipokea taarifa ya Utawala na Utendaji
kivita kutoka kwa Mkuu wa Kikosi cha Komando wakati wa ziara yake.
Amiri Jeshi Mkuu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.
Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akiangalia kupitia kilengeo maalum
kinachotumiwa kwenye silaha na makomando kulengea shabaha.
Makomando wakimuonesha Amiri Jeshi Mkuu na Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete (hayuko pichani)
mapigano bila shilaha wakati wa ziara yake.
Amiri Jeshi Mkuu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.
Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akifurahia mapambano ya kareti, taikondo na
judo yaliyokuwa yakioneshwa na makomando wa JWTZ
(Hawamo pichani).
Komando wa JWTZ akionesha uwezo wa kukwepa mapigo ya risasi za adui
kwa kupita juu ya mapigo hayo kwa kutumia kamba na kisha kuendelea na
jukumu alilopewa.
Kamanda wa Kikosi cha Uhandisi wa Medani akitoa taarifa ya Utawala
na Utendaji Kivita kwa (Hayupo pichani) mara baada ya Kikosi hicho
kutembelewa.
Amiri Jeshi Mkuu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.
Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akifafanua maeneo kadha ambayo Wahandisi
Medani wa JWTZ wamefanya kazi nzuri kurejesha miundombinu ya reli,
barabara na madaraja hata pale ambako Mamlaka za Kiraia zimekuwa na
maoni kuwa kazi hizo zingehitaji muda mwingi zaidi.
Amiri Jeshi Mkuu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.
Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akipewa maelezo kuhusu moja ya mitambo mipya
inaotumiwa na Wahandisi medani kusafisha maji chumvi na baridi na kuwa
maji safi na salama inayomilikiwa na Kikosi cha Uhandisi Medani.
Akipata maelezo kuhusu baadhi ya mitambo mipya ya kutengeneza barabara katika Kikosi cha Uhandisi Medani.
Amiri Jeshi Mkuu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.
Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akivuka juu ya daraja jipya la medani
lililojengwa kumuonesha uwezo wa Wahandisi Medani wa JWTZ kuendelea
kusaidia usafirishaji wa zana na vifaa hata pale madaraja ya kudumu
yanapoharibiwa kwa namna yoyote ile.
0 comments:
Post a Comment