Tuesday, March 4, 2014

8:40 PM



MWIGIZAJI mwenye sifa za kimataifa Evonne Cherryl ‘Monalisa’ amewashukia wasanii nyota wanaojisahau na kujiona kuwa wao ndio wao, na wanajitaidi kuwabania wasanii wengine wanaotaka kuingia katika fani hiyo, Monalisa anawashangaa wasanii hao ambao wanataka kumiliki tasnia hiyo kwa kibali cha nani?


Monalisa akiwa katika pozi matata


Monalisa akiwa na tuzo yake ya mwigizaji bora wa kike wa mwaka 2010


katika pozi
“Tasnia ya filamu kwa sasa imevamiwa na watu wasio na mbele wa nyuma, tena wenye roho mbaya ambao wanawabania hata wasanii waliotangulia kabla yao, hivi sisi kama tungewabania wao wasiingie kuigiza leo wangekuwa nyota? Kuwa msanii nyota si kuwa na majungu, fitina na roho mbaya,”analalamika Monalisa.
Monalisa anasema kuwa hivi sasa kuna tabia mbaya ambayo inafanywa na wasanii ambao hajawataja kwa majina, kuwa mara nyingi inapotakiwa kampuni mpya na kuitaji kufanya kazi ya filamu, wasanii hao wafikapoa katika kampuni hiyo uendesha vitendo vya chuki, majungu na kuwaponda wasanii wanaochaguliwa kwa ajili ya kazi husika huku wakijigamba kuwa wao ndio kila kitu.

0 comments:

Post a Comment