Monday, March 3, 2014

5:48 AM

Waigizaji wa filamu nchini ambao pia ni wanamuziki wa Bongofleva Hemedy Suleiman na Najma Datan wamezua maswali kwa watu wanaofuatilia habari za mastaa wa Tanzania baada ya picha zao wakiwa kimahaba zaidi kuanza kusambaa.
 Katika picha hizo zinazoonekana hapo juu  na chini wawili hao wanabusiana kimahaba kama wapenzi walioshibana. Haijajulikana kama picha hizo ni za video mpya ya muziki, filamu au ni wapenzi kweli.
Hata hivyo tayari inajulikana kuwa Hemedy kwasasa anatoka na Zuhura Gora ambaye ni model na muigizaji pia, huku Najma akiwa ameshawahi kuwa katika penzi na Mr.Blue, Najma pia hivi karibuni alijitosa Rasmi kwenye tasnia ya filamu Swahiliwood na filamu ya Fan’s Death akiwa na Vicent Kigosi(Ray) na Rammy Galis.

0 comments:

Post a Comment