Saturday, March 15, 2014

6:56 AM

Mtalaka ambaye ni Raia wa Uingereza  Amanda Rodgers ametoa kali ya mwaka baada ya Kufunga Ndoa na Mbwa wake kipenzi aliyempa Jina la Sheba baada ya kudai kuwa na mapenzi ya dhati na Mbwa wake huyo kwa muda mrefu sasa.


Amanda Rodgers ameolewa na Mbwa wake huyo (Sheba ) katika harusi iliyofana kwa namna ya kipekee huko Nchini Croatia katika hafla iliyohudhuriwa na watu takribanni 200.

Amanda Rodgers Akiwa na Mumewe Sheba
Amanda Rodgers Akiwa na Mumewe Sheba
Mtalaka huyo wa miaka 46 aliyekuwa amevalia kigauni chenye rangi nyeusi huku bwana harusi ambaye ni mbwa akiwa amevalia Shela Jeupe. Wapendanao hao walionekana kuwa na Nyuso za furaha huku Amanda Rodgers Akisisitiza kuwa Aliamua kufanya Uamuzi huo baada ya Kutengana na mumewe wa Ndoa miaka 20 iliyopita.

Amanda Rodgers Aliendelea kwa kusema:
“Mbwa huyu(Sheba) Nimekuwa nae Maishani kwa kipindi kirefu sana, yeye ndiye ambaye ananifanya nicheke, nifurahi na kunituliza pindi ninapojisikia vibaya”
mbwa2
Wanandoa hao baada ya Kufunga harusi
Sheba na Amanda Rodgers walimaliza harusi yao na kurejea Nyumbani kuendelea na Maisha ya Unyumba.

0 comments:

Post a Comment