Saturday, March 15, 2014

2:21 PM
 
 
 William [mwenye shati jekundu] dizaini huyo wa kushoto ndio mshindi wa pili.
 
William_Masvinu
Kama unakumbuka shindano la kumtafuta mtu mwenye sura mbaya kupita wote nchini Tanzania liliwahi kutokea na mshindi akaibuka jamaa mmoja anaitwa Masudi. Miongoni mwa watu ninaowakumbuka kushiriki shindano lile ni pamoja na Marehemu Remmy Ongala na Mzee Jangala ambaye enzi zile alikuwa muigizaji maarufu sana hususani katika vipindi vya radioni. Nakumbuka katika mchezo mmoja ambao ulinivutia na kuufuatilia sana alikuwa na mwanae wa kiume anayeitwa Mshamu.
Bahati mbaya shindano lile halijawahi kurudiwa tena. Masudi, ambaye baada ya kuibuka mshindi alidai anapata usumbufu mkubwa kutoka kwa “wachumba” wanaotaka awaoe, anabakia kuwa mtu mwenye sura mbaya kupita wote nchini Tanzania…kama kweli.
Hivi karibuni, nchini Zimbabwe, pengine kwa kufuata mfano ule wa Tanzania, nao wamekuwa na shindano la kumtafuta mwanaume mwenye sura mbaya kupita wote nchini humo.
Mshindi, kwa mwaka wa pili mfululizo, ameibuka kuwa William Masvinu unayemuona hapo pichani juu. Mbali ya kupewa zawadi ya mtoto wake mmoja kulipiwa ada ya shule, William pia alichukua dola za kimarekani $100. Tofauti na Masudi wetu, William tayari ana mke, Alice Chabhanga. William anasema mkewe ndio mwanamke pekee aliyemkubali na kwa sababu hiyo ana uhakika kwamba hana mshindani.
Alaa..hata “ubaya” una faida yake…
 
mr-ugly-contest

0 comments:

Post a Comment