Mume aliyejulikana kwa jina moja la Ngosha, mkazi wa Mabibo jijini Dar, amemfumania rafiki yake aitwaye Jazira akiwa chumbani na mkewe Jack wakiivunja amri ya sita ya Mwenyezi Mungu.Tukio hilo lilitokea Jumanne iliyopita saa 12 alfajiri ambapo ilidaiwa kuwa Jack alikuwa chumbani na mwanaume huyo ambaye ni mpangaji, wenzake wakipeana maraha.
Imedaiwa
kuwa, wawili hao walikuwa wakimtegea Ngosha akitoka kwenda katika
shughuli zake, Jazira alikuwa akizama katika chumba cha rafiki yake na
kufanya mchezo wa kikubwa.
Wapangaji
wenziye na Jack wamedai kuwa, mke huyo wa mtu ambaye ana miezi miwili
tangu aolewe kutoka mkoani Tabora, amekuwa kero katika nyumba hiyo kwani
amekuwa akipiga kelele za kimahaba nyakati za asubuhi ambapo watu wengi
wanakuwa wakielekea kazini.
“Hata
sisi wanawake tunaoishi nyumba hiyo tuna waume zetu tunawalilia lakini
kinachotusikitisha mwenzetu anamlilia Jazira badala ya mumewe ambaye
anakuwa amekwenda kazini,” alisema mmoja wa wapangaji wa nyumba hiyo.
Imeelezwa kuwa, siku hiyo mlinzi wa msikiti alikwenda kumwamsha Ngosha kwenda kusogeza gari lake ili watu wapite na alipofika katika chumba chake, alikuta mlango wa sebuleni ukiwa wazi lakini hakukuwa na mtu, ila chumbani kwake kulisikika redio ikizungumza kwa sauti kubwa.
Jirani mmoja aliyedai kuchoshwa na tabia hiyo, alimshauri mlinzi huyo
kwenda kusikiliza kwenye dirisha la chumba hicho na waliposikia sauti za
kimahaba wakakubaliana wamtonye mjumbe wa Serikali ya Mtaa wa Kanuni,
Mabibo aliyetajwa kwa jina la Asha ambaye alifika na kusikia ‘mchezo’
ukiendelea chumbani.
Wakati huohuo, Ngosha akapigiwa simu kuja kushuhudia mchezo huo mchafu wa mkewe alioufanyia ndani ya chumba chake.
Mashuhuda wa tukio hilo walisema, alipofika Ngosha nyumbani na kutonywa
kilichotokea alipandwa na hasira na kuangusha varangati kwa rafiki
yake lakini baadaye akatulizwa, akamtaka Jazira amlipe shilingi milioni
1.2 ili amuachie mke moja kwa moja.
JAZIRA ANA LAKI 2
Jazira
alisema hakuwa na kiasi hicho isipokuwa anaweza kulipa shilingi laki
mbili tu, jambo lililomfanya Ngosha kuomba msaada wa askari mgambo na
kumpeleka mgoni wake Kituo cha Polisi cha Urafiki kwa ajili ya hatua
zaidi za kisheria.
CREDIT: GPL
0 comments:
Post a Comment