Saturday, December 7, 2013

2:33 AM
Hatimaye raisi wa SA Bw. Jacob Zuma ametangaza rasmi kwamba marehemu Nelson Mandela atazikwa 15/12/2013 kijijini kwake Qunu katika jimbo la Eastern Cape. Bendera za SA zitapepea nusu  mringoti kwa muda wa siku 10 na ametangaza 08/12 kila mwaka kuwa siku ya kumbukumbu ya mzee Mandela. Sala ya mazishi imepangwa kufanyika December 10, 2013 katika uwanja wa taifa wa FNB huko Johanesburg. Mwili wake utawekwa katika jengo la serekali liitwalo Union buildings kuanzia December 11 hadi 13 kwa kupewa heshima za mwisho.
uwanja wa Taifa ambako mwili wa Mandela utaagwa.


Jengo Union Building ambako mwili wa Marehemu utawekwa kwa kuagwa.

ulinzi ukiwa umeimarishwa nyumbani kwa Marehemu.

0 comments:

Post a Comment