Wednesday, December 4, 2013

6:35 AM
Selemani Msindi aka Afande Sele ambaye hivi karibuni alitangaza kujiunga na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) (Taarifa hizo zilikanushwa na viongozi wa CHADEMA mkoa wa morogoro), ametoa maoni yake kuhusu vuguvugu linaloendelea katika chama hicho na uamuzi wa kumvua Zitto Kabwe nyadhifa zote katika chama hicho.
Afande Sele ameiambia tovuti ya Times FM kuwa anakishauri chama hicho kutumia busara zaidi kuliko kuangalia zaidi maamuzi ya watu wachache ama kujikita zaidi kwenye vifungu vya sheria na katiba yao.
“Kilichomtokea Zitto, mtu ambaye naamini amesimama tangu mwanzo hadi chama kimefikia hapa, kwangu mimi nadhani chama kinapaswa kutumia busara sana kulikabiri hili tatizo. Kwa sababu mwisho wa siku kama tutashupaza shingo unaweza kujikuta linavunjika. Mi nafikiri chama kinatakiwa kukaa chini na kutumia zaidi hekima na busara kuliko kuangalia tu maswala ya kanuni na maamuzi ya watu wachache.” Amesema Afande Sele.

                     Afande Sele aka Mfalme wa Rymes akiwa kwenye pozi.

Mbali na maoni hayo, King Selemani wa Morogoro au unaweza kumuita Mtu Pori, alitoa angalizo.
“Nafikiri ni chama kizima kujitazama na kuhakikisha kwamba tulipofikia hapa na kinachotokea kwenye  chama  kinaweza kusambaratisha chama, na kama chama kitasambaratika ni wazi hata nchi yenyewe haitakuwa salama kwa vile upinzani makini husababisha serikali makini, na kama upinzani ukiwa mbovu ina maana hata serikali haiwezi kuwa sawa.”
Usikose kusikiliza The Jump Off ya 100.5 Times Fm kwa habari zaidi na ngoma kali kuanzia saa mbili kamili usiku hadi nne kamili usiku.

0 comments:

Post a Comment