Wednesday, December 4, 2013

7:00 AM
Mahakama ya rufaa kanda ya Dar es Salaam imeridhia hukumu iliyotolewa na hakimu wa Mahakama ya Hakimu mkazi Kisutu ya faini ya Tzs 13 Millions dhidi ya msanii Kajala Masanja. Kwenye hukumu hiyo ya hakimu makazi star huyo wa Bongo Movies, Kajala Masanja, aliwekwa huru na mahakama hiyo baada ya kulipa pesa hiyo ili kukwepa kifungo cha jela.
                                             Kajala akivinjari maeneo ya jiji la Dar es Salaam

 Hata hivyo baada ya kutoridhika na hukumu hiyo, aliyekuwa mumewe, Bw. Faraji Augustino alikata rufaa dhidi ya maamuzi hayo ya mahakama. Rufaa hiyo ilisikilizwa na  kuridhia maamuzi ya mahakama ya hakimu mkazi Kisutu. Kuridhika huko kunamaanisha Kajala sasa yuko huru. Aliyekuwa mumewe Kajala, Bw. Faraji Augustino, anatumikia kifungo cha miaka mitano jela baada yakukutwa na hatia ya kutakatisha fedha haramu mapema mwaka huu, 2013.

0 comments:

Post a Comment