Sunday, December 8, 2013

1:44 AM
Sehemu ya chini ya meli hiyo
Meli hiyo inavyoonekana kabla ya kuzama
Meli hiyo ilipoanza kuzama
Meli  hiyo kama inavyoonekana kwa juu baada ya kuzama kabisa ndani ya maji


Meli ndogo ya mizigo ya MV MERCI II inayomilikiwa na Semuhungu Shingiro imezama katika bandari ya Kilwa masoko. Mtu mmoja aliyefahamika kwa jina la Nice Mtega fundi mkuu wa meli hiyo anahofiwa kufa maji baada ya kutoweka kwa zaidi ya masaa 36 toka kuzama kwa meli hiyo.
Akiongea na Michuzi Blog, Meneja wa Bandari ya Kilwa, Bw. Iddi Omary, alieleza kuwa meli hiyo iliyofunga gati jana jioni ikitokea Songosongo na  kupakia tani 30 za mchanga na tani 30 za maji ilizama majira ya saa 6 usiku wa kuamkia leo ambapo nahodha wake Charles Kalinga na wasaidizi wake watatu walifanikiwa kutoka ila Nice Mtega aliyekuwa ndani hajaonekana hadi sasa.
Juhudi za kumtafuta na kuinua meli hiyo zinaendelea. Sababu ya kuzama kwake bado hazijajulikana.
Source: global publishers

0 comments:

Post a Comment