Tuesday, February 25, 2014

7:42 AM


Wagoni Wauawa kwa Mawe.

Wagoni wawili Wanaokadiriwa kuwa na Miaka 30 kila mmoja Wameuwa Kikatili baada ya Kunaswa Wakishiriki Vitendo vya Ngono. Inasadikiwa Kuwa wagoni hao Kila mmoja na Ndoa yake na Kitendo cha Kunaswa Wakivunja Amri ya Sita Imewaghadhabisha Mno Raia wa Baluchistan Magharibi mwa Pakistan.

Aidha waliohusika na Mauaji ya Wagoni hao Wawili wamekamatwa na Polisi kwa Kosa la Mauaji, Baba na Kaka wa Mwanamke Pamoja na Mjomba wa Mwanaume wanashikiliwa na Polisi kwa Kosa Hilo la Mauaji.


Wagoni Wakiuawa kwa Kupigwa Mawe
“Ni kitendo cha Kikatili sana na Watu waliohusika na Mauaji haya ni Lazima Wafikishwe mbele ya Sheria” Alisema Bugti Ambaye ni Balozi wa Eneo Hilo la Magharibi mwa Pakistan

Hali ya Hatari.

Taarifa Zinaeleza Kuwa Kumekuwa na Ongezeko la Matendo ya Kinyama yanayofanyika Nchini Humo Hadi Kufikia Kiasi cha kesi 1000 kila Mwaka huku kukiwa na hofu ya Idadi Hiyo Kuzidi Kuongezeka Zaidi

0 comments:

Post a Comment