Wednesday, February 26, 2014

10:45 PM

Ufuska mtupu! Mnenguaji wa kiume wa Bendi ya African Stars ‘Twanga Pepeta’, Bakari Kisongo ‘Mandela’ ametoa kali ya kufungia mwaka baada ya kunaswa ‘laivu’ akililia penzi kutoka kwa dada aliyetajwa kwa jina moja la Zainab.


Bakari Kisongo ‘Mandela’ (kushoto) ametoa kali ya kufungia mwaka baada ya kunaswa ‘laivu’ akililia penzi kutoka kwa dada Zainab.
Tukio hilo la aina yake lililoshuhudiwa na ‘fotografa’ wetu lilitokea juzi nje ya Ukumbi wa Mango Garden, Kinondoni jijini Dar ambapo Twanga ilikuwa ikivurumisha burudani ya Sikukuu ya Krismasi.

Bakari Kisongo ‘Mandela’ (kushoto) akilazimisha penzi.
Mara baada ya bendi hiyo kumaliza kufanya onesho lake majira ya saa 9:30 usiku, mnenguaji huyo alionekana akizama kwenye Baa ya Uhuru Peak inayotazamana na Mango kisha akamwita msichana huyo ili waondoke
Kwa mujibu wa mashuhuda waliokuwa karibu, kulitokea kama mtafaruku kwani msichana huyo alikataa katakata kuondoka na mnenguaji huyo.
Baada ya kuona hivyo, Mandela alitumia mbinu mbadala (nguvu) ambapo alimvutia mrembo huyo ndani ya Bajaj iliyokuwa imepaki eneo hilo ndipo mtafakuru ukazuka.
Huku na huku, dada huyo alipata upenyo ambapo alichoropoka na kutoka nje ambapo Mandela naye alimrukia na kuanza kumlilia huku akilazimisha mambo ya kikubwa hadharani ikiwepo ‘kudendeka’.
Hata hivyo, Mungu mkubwa kwa sababu mrembo huyo alifanikiwa kumtoka Mandela kisha akadandia Bajaj nyingine na kuondoka kwa kasi huku akimwacha jamaa na mfadhaiko.
Mashuhuda wa tukio hilo walimponda Mandela wakidai kuwa huo ni ufuska kwani kitendo alichotaka kufanya si cha kuigwa katika jamii.
Gazeti hili lilipomtaiti Mandela kutaka kujua kulikoni kuomba mambo ya kikubwa hadharani hakuwa na la kusema zaidi ya kusikitika kumkosakosa mrembo huyo.


0 comments:

Post a Comment