Wednesday, February 26, 2014

6:14 AM


AMA kweli shetani anafanya hesabu zake za mwisho! Tangu mwaka 2014 uanze yapo yaliyotokea na kusisimua likiwemo la kunaswa kwa kinara wa utoaji mimba, Dk. Mambo, maeneo ya Kawe, Dar lakini hili la warembo kufumwa wakitoa dozi ya ngono linaweka historia nyingine, Ijumaa linaibumburua
Warembo wanaotoa huduma wakiwa wameficha sura zao baada ya kunaswa na OFM.
Hebu sikia, saluni inayojihusisha na vitendo vya ’masaji’ lakini kumbe ngono imo ndani yake imenaswa na kufumuliwa baada ya kukutwa uchafu wa aina yake nyuma ya pazia.

Saluni hiyo maarufu kuliko Miji ya Sodoma na Gomora, ipo maeneo ya Sinza ambapo kwa muda mrefu sasa imekuwa ikijihusisha na uchafu huo na kusababisha kero kwa wananchi wenye maadili yaliyotukuka.
TAARIFA MEZANI
Oparesheni Fichua Maovu (OFM) chini ya Global Publishers, ikiwa imetulia ndani ya mjengo wa makao yake makuu, Bamaga-Mwenge jijini Dar, Mkuu wa kikosi maalumu cha Mtambo wa Kurekebisha Tabia (MKT) ambacho ni kitengo ndani ya OFM, alipokea simu kutoka kwa msamaria mwema akitoa ‘tipu’ juu ya ishu hiyo.

0 comments:

Post a Comment