Friday, February 28, 2014

2:49 AM

Ni siku chache zimepita tangu PNC atangaze rasmi kujitoa Mtanashati Entertainment na kujiunga na crew nyingine ambayo nayo ikatangaza kufurahia kwake kumpata msanii huyo ambaye walidai na recording za ngoma zao zimeshaanza.
Lakini siku ya jana Big Boss wa Mtanashati ambaye ni Ostazi Juma aliweka wazi kwenye mitandao ya kijamii juu ya tukio la kurudi kwa PNC na kumuomba msamaha na kuhitaji arudi tena kundini. Kama haitoshi kuweka wazi huko kuliambatana na maneno haya

Status ya kwanza: “hahaha jamani mziki ni kazi pnc arudi kuomba msamaha ili aendelee kufanya kazi mtanashati.”
Status ya pili: “jamani mziki ni mgumu sana, pnc karudi kwa kuomba msamaha kwa boss wake Ostaz juma.”
Mbali na picha hizo ambazo zimeleta gumzo kubwa mitandaoni haikuishia hapo bali Ostaz alitupia na video inayochukua sekunde kumi na sita inayomuonesha PNC akiomba radhi kwa bosi wake huyo wa zamani ili arudi kwenye usimamizi wa Mtanashati Entertainment.

0 comments:

Post a Comment