Wednesday, February 26, 2014

3:20 PM

Madiwani wawili wa Chadema kutoka Kata ya Ngokolo, Sebastian Peter na wa Kata ya Masekelo, Zacharia Mfuko zilizopo Shinyanga Mjini wametangaza kukihama chama hicho na kujiunga CCM.
Kutokana na hali hiyo, Katibu Mkuu wa Chadema, Dk Wilbroad Slaa amekituhumu CCM kwa mchezo mchafu.

Awali CCM inadaiwa kuanza mkakati wa kuwachukua waliokuwa viongozi wa chama hicho waliofukuzwa uanachama hivi karibuni wilayani Kahama kwa tuhuma mbalimbali ikiwemo kumuunga mkono aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu wake, Zitto Kabwe.

Katika mikakati hiyo, juzi kiongozi wa juu wa Umoja wa Vijana Taifa (jina tunalo), aliingia mjini Kahama kimyakimya na kufanya mkutano wa siri na waliokuwa viongozi hao.
Chanzo cha habari kilidai kuwa kiongozi huyo baada ya kufika mjini Kahama akitokea Dodoma alifikia hoteli mojawapo mjini Kahama kwa siri na kualika baadhi ya makada wachache wa CCM ambao aliwapa masharti ya kutotoa taarifa yoyote juu ya ujio wake Kahama.

Viongozi hao waliofukuzwa ni pamoja na Diwani wa Kata ya Majengo, Bobson Wambura, Mwenyekiti wa Jimbo la Kahama, Israel Barakiel, Katibu wa jimbo hilo, Vicent Kwilukilwa, Mwenyekiti wa Bavicha Jimbo, Benedicto Shija, Mwenyekiti Bawacha Jimbo, Kasigwa Adram pamoja na Mratibu wa Vijana Wilaya, Vicent Manyambo.

Hata hivyo, Dk Slaa akihutubia mkutano wa kampeni za kumnadi mgombea wa Chadema, Grace Tendega alisema anatoa ruksa kwa wabunge na madiwani wasiopenda kutumikia wananchi kuondoka Chadema.

0 comments:

Post a Comment