Shirikisho
la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) na Kocha wa Taifa Stars, Kim Poulsen
wamekubaliana kuvunja mkataba katika makubaliano ambayo ni siri kwa
pande zote mbili.
Uamuzi
huo ulitangazwa jana (Februari 27 mwaka huu) jijini Dar es Salaam kwa
pamoja na Rais wa TFF, Jamal Malinzi na Kocha Poulsen mbele ya waandishi
wa habari.
Rais
Malinzi kwa niaba ya TFF ametoa shukrani za dhati kwa Kocha Poulsen kwa
ushirikiano na mchango ambao ameutoa kwa Tanzania kuanzia kwenye mpira
wa miguu wa vijana.
Naye
Kim amewashukuru Watanzania kwa ushirikiano waliompatia kwa kipindi cha
miaka mitatu alichokaa nchini kuanzia Mei 2011 alipoteuliwa kuwa kocha
wa timu za Taifa za vijana, na baadaye Taifa Stars.
Akizungumzia
benchi jipya la ufundi la Taifa Stars, Rais Malinzi amesema
linatarajiwa kutangazwa hivi karibuni likiongozwa na kocha kutoka nje ya
Tanzania.
Amesema
kwa upande wa mechi dhidi ya Namibia itakayochezwa Machi 5 mwaka huu
jijini Windhoek, Stars itaongozwa na Kaimu Mkurugenzi wa Ufundi, Salum
Madadi akisaidiwa na kocha Hafidh Badru kutoka Zanzibar.
Katika
hatua nyingine, Kocha Madadi amewaondoa wachezaji watano wa Yanga
katika kikosi kilichotajwa awali ili wapate fursa ya kuitumikia timu yao
kwenye mechi mbili za Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Al-Ahly ya
Misri.
Wachezaji
hao ni Athuman Idd, David Luhende, Deogratius Munishi, Frank Domayo,
Kelvin Yondani na Mrisho Ngasa. Pia kipa Ivo Mapunda ameondolewa katika
kikosi hicho baada ya kupata msiba.
Nafasi
zao zimezibwa na wachezaji Abdi Banda (Coastal Union), Himid Mao
(Azam), Juma Luizio (Mtibwa Sugar), Said Moradi (Azam) na Shabani Kado
(Coastal Union).
0 comments:
Post a Comment