Ugonjwa wa homa ya nguruwe umelipuka tena mkoani Mbeya na kuua zaidi ya nguruwe 900 katika wilaya za Mbeya na Rungwe.
Mganga
Mkuu wa Mifugo Mkoani Mbeya, Solomon Nong’ona akizungumza nasi jana
alisema, ugonjwa huo umerudi tena baada ya kuzuka kwa mara ya kwanza
Januari mwaka huu na kutokomezwa.
Alisema
kufuatia kuzuka tena kwa ugonjwa huo, serikali kupitia sekta ya mifugo
imepeleka dawa mkoani humo ambazo zinasaidia kupunguza kasi ya kuenea.
Nong’ona
alisema kufuatia kuzuka kwa ugonjwa huo wananchi nao wanajitahidi
kununua dawa hizo ili kuudhibiti na kuwakinga nguruwe wanaowafuga.
0 comments:
Post a Comment