Mwimbaji mkongwe wa muziki wa dansi nchini, Ramadhan Masanja ‘Banza Stone’ amefunguka mazito juu ya matumizi mabaya ya bangi na madawa ya kulevya ikiwa ni pamoja na jinsi alivyokuwa akiyatumia.
Akizungumza
kupitia Kipindi cha Mtu Kati cha Global TV mwanzoni mwa wiki hii,
Banza alikiri kutumia madawa ya kulevya na kusema; “Nilianza kuvuta
sigara ya kawaida, nikaja bangi na baadaye madawa ya kulevya aina ya
Heroin ambapo alikuwa akiyatumia kwa kuchanganya na sigara au bangi.
“Ujana
ulisababisha nikajiingiza katika matumizi ya madawa ya kulevya ila sasa
nimeacha kabisa na nawashauri vijana wenzangu kuwa mbali na kilevi
hicho kwani kama huna kipato cha kutosha unaweza kugeuka kibaka maana
mwili ukizoea ni vigumu kuacha.”
0 comments:
Post a Comment