Balozi Kazaura
Rais Mstaafu, Benjamin Mkapa
alikuwa miongoni mwa maelfu ya waombolezaji waliofika katika ibada ya
kuaga mwili wa Balozi, Fulgence Kazaura aliyefariki dunia mwishoni mwa
wiki akiwa katika matibabu nchini India.
Ibada
hiyo ilifanyika katika Kanisa Katoliki la Mt Peter, Oysterbay jijini,
na kuhudhuriwa na viongozi wa chama na Serikali, mabalozi mbalimbali
Tanzania waliokuwa wanafanyakazi nje ya nchi kupitia Chama cha Mabalozi
Wastaafu (ACTA), wakurugenzi, wanazuoni na wahadhiri wa Chuo Kikuu cha
Dar es Salaam (UDSM).
Akizungumza
wakati wa ibada hiyo, mtoto wa marehemu, Kamugisha alisema kuwa baba
yao alifariki kutokana na ugonjwa wa saratani ya koo ambayo ilianza
kumsumbua tangu mwaka 2012 na iligundulika Juni mwaka jana.
Alisema
kuwa baba yao alikuwa akilalamika kushindwa kumeza chakula na baada ya
kuhangaika na matibabu katika hospitali mbalimbali nchini, Juni mwaka
jana walimpeleka nchini India alikobainika kusumbuliwa na ugonjwa huo.
“Walimtibia
na alikuwa anaelekea kupata nafuu kwani walau alirejea katika hali ya
kawaida ingawa siyo kama awali” alisema na kuongeza kuwa ilipofika
Agosti hali ikabadilika ikabidi wamsafirishe tena nchini India ambako
alitibiwa kwa miezi miwili kisha kurudi nchini.
Alisema
hali ilibadilika tena Oktoba mwaka jana ndipo akarudishwa nchini India
ambako walimfanyia uchunguzi na kugundulika kuwa saratani ilikuwa
imesambaa sehemu zingine.
Kwa
mujibu wa ratiba ya maziko, mwili wa marehemu utaagwa leo kwenye Ukumbi
wa Nkrumah wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), kabla ya
kusafirishwa kwenda kijiji alichozaliwa cha Igurukati, Bugandika mkoani
Kagera kwa ajili ya mazishi yatakayofanyika Jumamosi.
Kabla ya umauti, Balozi Kazaura
aliyezaliwa 11 Septemba,a 1940, alishika nyadhifa mbalimbali kama
Ukatibu Mkuu wizara mbalimbali na kuwa balozi wa Tanzania Ulaya (EEC).
Viongozi
wa Kanisa hilo la Mt. Peter wakiwaongoza waomboleazaji kuaga Mwili wa
aliyekuwa Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Marehemu Balozi Kazaura aliefariki Dunia juzi huko nchini India alikokwenda kwa ajili ya Matibabu.
Rais
Mstaafu wa awamu ya tatu,Mh. Benjamin Mkapa akiwaongoza waomboleazaji
mbali mbali kutoa heshima za mwisho wakati wa kuaga Mwili wa aliyekuwa
Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Marehemu Balozi Kazaura
aliefariki Dunia juzi huko nchini India alikokwenda kwa ajili ya
Matibabu
Waziri
Mkuu Mstaafu,Jaji Joseph Warioba akitoa heshima za mwisho kwa Mwili wa
aliyekuwa Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Marehemu Balozi
Kazaura aliefariki Dunia juzi huko nchini India alikokwenda kwa ajili ya
Matibabu
Kaimu
Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM),Prof. Rwekaza Mkandala
(mbele) Sir George Kahama,pamoja na Makamu Mwenyekiti wa CCM Bara,Mzee
Phillip Mangula wakitoa heshima zao za Mwisho kwa Mwili wa aliyekuwa
Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Marehemu Balozi Kazaura
aliefariki Dunia juzi huko nchini India alikokwenda kwa ajili ya
Matibabu
0 comments:
Post a Comment