CHAMA cha Mapinduzi (CCM)
CHAMA cha Mapinduzi (ccm),
kimejiingiza matatani baada ya kuwapangisha wafanyabiashara wawili
katika flemu moja la kufanyia biashara. Akizungumza jana jijini Dar es
Salaam mfanyabishara Charles Msigwa alisema aliingia mkataba na Mecy
Mziray ambaye kwa sasa ni marehemu na aliendelea kumlipa kodi ndugu wa
marehemu Vesta Haule. Alisema wakati akiendelea kufanya biashara katika
banda hilo alishangazwa na viongozi wa CCM tawi la Vigaeni Kata ya
Ndugumbi kumfuata wakitaka aingie mkataba upya na chama hicho.
Msigwa Afunguka
“Nimekuwa nikiendesha shughuli zangu za biashara kwa muda wa miaka
minne ndipo nilipofuatwa na viongozi wa CCM na kunishauri nichukue
mkataba nao ili chama kipate mapato,”alisema Msigwa.
Aliongeza kuwa viongozi hao walimuita kwenye ofisi ya tawi na
kumuhakikishia hakutakuwa na tatizo lolote juu ya mkataba huo. “Viongozi
hao waliniambia kuwa mabanda hayo hayarithishwi hata hivyo aliyeachiwa
amekuwa msumbufu wa kodi mwenye banda alishafariki kwa hiyo banda huwa
linarudi na kuwa mali ya chama,”alisema.
Msigwa alisema kuwa aliujaza mkataba huo na kuurudisha ofisini kwao
alipotaka kuulipia akawa anazungushwa zungushwa. “Nilipeleka malalamiko
yangu Kwa uongozi wa Wilaya ambapo uliwaandikia barua ya kwamaba
wanitafutie banda jingine iwapo nikiwa tayari kutimisha masharti ya kuwa
mpangaji wa chama hicho na nilikubali lakini uongozi huo haukufanya
kama ulivyo agizwa,”alisema Msigwa.
Awali Chama cha mapinduzi (CCM)
kiliingia mkataba wa kujenga banda hilo na Marehemu Mecy Mziray gharama
zake na asingeweza kutoka mpaka gharama zake za ujezi zitakapo
malizika.
0 comments:
Post a Comment