Umuzi
huo ulitolewa jana na Jaji , Rose Teemba baada ya kusikiliza hoja za
pande zote mbili kuhusu maombi ya marejeo ya kupinga kuondolewa shitaka
hilo yaliyowasilishwa mahakamani hapo na Sheikh Ponda.
Kabla
ya uamuzi huo kutolewa upande wa Jamhuri ukiongozwa na Wakili wa
Serikali Mkuu Benard ess Zakaria, walidai kuwa wanapinga maombi hayo
kusikilizwa kwa sababu kiapo kilichoambatana nayo kinamapungufu ya
kisheria.
Kongola
alidai kuwa kiapo kinabeba hoja za maneno ya maombi hayo na kwamba kama
kimekosewa yatakuwa batili hayafai kusikilizwa na mahakama yatupwe.
“Katika
hati ya kiapo hicho hakuna baadhi ya vipengele ikiwemo tarehe ya
kuwasilisha kiapo na muapaji aliapa kwa mtu anayemfahamu au
alitambulishwa na nani… kosa hilo haliwezi kurekebishika kwa hiyo maombi
yaliyopo mbele yako Mtukufu Jaji ni batili” alidai Kongola wakati
akitoa hoja za kupinga maombi ya Ponda yasisikilizwe.
Akifafanua
zaidi wakili huyo alidai kuwa Jamhuri inapinga maombi hayo kusikilizwa
kwa sababu yamekiuka kifungu namba 8 cha sheria inayosimamia viapo.
Akijibu
hoja za Jamhuri, wakili wa utetezi Juma Nassoro alidai kuwa pingamizi
la Jamhuri halina misingi ya kisheria na kwamba kiapo kinaonyesha maombi
yaliwasilishwa Oktoba 10, mwaka 2013.
Juma
alidai kuwa aliyekula kiapo hicho ni Obadia G. Hamidu na mtoa kiapo
aliyetajwa kwa jina moja, Kifunda ni wakili anayemfahamu muapaji vizuri
na kwamba hoja za utetezi ni sahihi kwa mujibu wa kifungu namba 8 cha
sheria inayosimamia viapo.
Baada ya mabishano hayo ya kisheria Jaji Teemba alisema uamuzi wake utatolewa Desemba 11, mwaka huu.
0 comments:
Post a Comment