Saturday, December 7, 2013

2:08 AM

Kumekuwa na maswali mengi sana juu ya kimya kikubwa cha msanii wa R&B nchini Mohammed also known as MB Dog, mmoja kati ya wasanii wakali wa R&B waliwahi kuibuka around 2004 na kupotea ghafla 2008 kutokana na vikwazo mbali mbali alivyokutana navyo katika sanaa. Ngoma ya mwisho kuiachia ilikuwa Nikimtafuta aliyoitoa kabla ya kukimbia na kwenda kutafuta maisha nchi za nje.
Mb Dog aliondoka nchini 2009 kwenda England then later German alikokaa almost miaka miwili.Baada ya kufika Uingereza Mb Dog alipokelewa na rafiki yake anayeitwa Steve ambaye ni Dj, alikaa na rafiki yake huyo kwa miezi nane mjini Manchester huku akizungumzia maisha ya huko yakiwa ya kawaida sana tu japo aliweza kufanya baadhi ya show lakini hayakuwa mazuri sana na baadae kijana huyo aliyefanya vizuri sana Tzee aliamua kubadili upepo na kwenda nchini Ujerumani.

Baada ya kurudi nyumbani alipata tena mchongo mwengine wa kwenda Ujerumani hiyo ilikuwa 2010 na huko pia maisha yakawa ya kawaida kwani alikutana na watanzania wengi sana wanaotafuta maisha kama yeye na hakuona tofauti wa maisha ya Uingereza na yale ya German.
Huku akiweka wazi faida chache alizozipata akiwa huko ni kufanikiwa kupata show almost 12 katika miji toufauti  ya Amsterdam, Munich na miji mingine.
Mbali na mafanikio hayo but Mb Dog aliweza kutengeneza Ngoma mbili akiwashirikisha wasanii tofauti kama I miss you alifanya na  Clow kutoka Munich na ngoma nyingine inayoitwa Nchi yangu.
Alivyojipanga kwa sasa, Mb Dog ameshatengeneza ngoma 15 kwa ajili ya kuzitambulisha kwa mashabiki wake baadhi ya ngoma hizo ni ‘Uzuri wa kwenda ni kurudi‘ na ‘Mama Digina’ na mkono hatari unaoenda kwa jina la Tanga tuzitegemee kuzisikia kwenye radio waves soon.
Huku akiwa mbioni kufungua studio yake na kila kitu akikamilisha nyumbani kwake” nina studio ina kila kitu, ila bado sijaamua kuanza kuvitumia mpaka pale nitakapo pale producer anayefanana na wale wakali kama Man Walter, Chizen Brain.
Mkali huyo mwenye watoto wawili Warda na Digina huku akiwa karibu sana na mama yake mzazi anayeishi hapa hapa mjini

0 comments:

Post a Comment