MSANII
maarufu wa Bongo Movie, mrembo na mwenye pesa pengine kuwazidi wengi na
ambaye hivi karibuni amezua mijadala mikubwa baada ya
kurudiana na mpenzi wake wa zamani Diamond, ambaye pia ni maarufu
katika muziki wa kizazi kipya nchini na mwenye kuongoza kwa mapato
nchini, imegundulika kuwa ana ujauzito wa miezi kadhaa.
Wema
ambaye alishindwa kuficha hisia zake na hatimae kuweka kuandika kwenye
mtandao wa kijamii wa instagram,” …mmmmmh jamani hichi kitumbo…
hakifichiki now…” kuashiria kuwa mabadiliko ya mwili yameshaanza
kuonekana (Picha chini inaonesha ujumbe huo kamili).
Mtandao huu ulianza kuhisi taarifa hizo na kuamua kuzifuatilia kwa karibu
ili kujua nini haswa kinaendelea au ni hisia tu. Ndipo mwandishi
alipochukua jukumu la kumtafuta mlimbwende huyo Wema Sepetu na kugonga
mwamba.
Hata hivyo jitihada hizo hazikuishia hapo ndipo
kilipopatikana chanzo cha karibu na Wema na kudai kuwa “ amekuwa
akilalamika mabadiliko hayo na hata kusikika akisema anaihisi
ameconsive…” kilisema chanzo hicho bila kutaka kutambulika hadharani.
“Ni kweli itakuwa hivyo na ndio maana Diamond aliamua kumtangaza rasmi siku hile ya chrismas” aliongeza.
0 comments:
Post a Comment