WAKATI binadamu wakiendelea na mipango yao ya kuifanya
dunia kuwa sehemu salama ya kuishi kimazingira, kiulinzi na usalama, utabiri
mpya wa kutisha unaonesha kuwa mwaka 2032 ndiyo mwisho wa sayari hii ya tatu
katika mfumo wa jua. Kwa mujibu wa vyanzo mbalimbali katika mitandao ya
internet, sayari iitwayo Nibiru, ambayo kisayansi inafahamika kama Planet X ipo
njiani kuigonga dunia na hivyo kusababisha majanga mbalimbali kutokea.
ITAONEKANA ANGANI KAMA
MWEZI
Kwa mujibu wa mitandao hiyo ya kisayansi, sayari hiyo ambayo inaisogelea dunia
kwa kasi kubwa, itaonekana kubwa na angavu wakati wa usiku angani na kuwa
katika umbo la mwezi na hivyo kufanya miezi ionekane miwili.
DALILI KWAMBA IPO JIRANI
Taarifa zaidi za kisayansi zinasema kuwa, kadiri sayari hiyo inavyozidi
kusogea, dunia itaanza kutikisika na kusababisha matetemeko ya ardhi kuongezeka
sehemu mbalimbali.
Mbali na dunia kutikisika
na matetemeko, milipuko ya volcano nayo itatokea huku idadi kubwa ya milipuko
hiyo mipya ikiongezeka, vimbunga vikubwa kama Tsunami vitaibuka na mwishowe
dunia itapigwa na bomu la miamba midogo na vimondo kutokea angani.
DUNIA ITAKUMBWA NA GIZA
NENE
Wakati volcano zote duniani zitakapoanza kulipuka na zingine mpya kujitokeza,
dunia itafunikwa na giza nene na matope kwa wakati wote wa usiku na
mchana huku watu wakitakiwa kusoma katika Biblia Joel 2: 1-2 na Zephaniah
1:14-17.
NI TUKIO LA AINA YAKE KARNE
YA 21
Nibiru inatajwa kama kitu kinachoisogelea dunia kinachoaminiwa kusababisha
madhara makubwa ambapo kama hakitaigonga dunia, kitasababisha mtikisiko usio wa
kawaida kitakapopishana nayo. Baadhi ya wanasayansi wanaamini kuwa kitendo
hicho kitatokea mapema katika karne ya 21 (tuliyonayo sasa).
WANASAYANSI WAPINGANA
Baadhi ya wanasayansi wanapinga kwa maelezo kwamba hakuna ushahidi wowote wa
kitafiti unaoonesha wazi kwa mabingwa wa anga za juu waliobobea wa masuala ya
nyota.
MWANAMKE ALIWAHI KUOTA
NDOTO
Kwa mara ya kwanza jambo hilo lilitokea mwaka 1995, wakati mwanamama Nancy
Lieder muasisi wa mtandao wa ZetaTalk, aliwahi kudai kuoteshwa ndoto kwamba,
Mei 2003 kuna kitu kitaingilia mfumo wa jua (solar system) na kusababisha dunia
kutoboka tundu litakalosambaratisha sehemu kubwa ya kizazi cha binadamu.
Lieder aliifafanua kuwa,
kitu hicho kitakuwa na ukubwa wa mara nne ya dunia.
BAADA YA NDOTO
Baada ya mwanamama Lieder, mtu wa kwanza kuizungumzia Nibiru alikuwa Mark
Hazlewood, mwanachama wa zamani wa mtandao wa ZetaTalk ambaye mwaka 2001
alichapisha kitabu kilichoitwa Blindsided na kusema kuwa mwisho wa dunia
ungekuwa mwaka 2003 baada ya kuwasili kwa sayari ya kumi (Nibiru).
Katika mfumo wa sasa,
baadhi ya wanasayansi wanasema sayari ziko 12, wakizitaja kwa namba 1. Jua 2.
Mercury 3. Venus 4. Dunia 5. Luna (mwezi) 6. Mars 7. Jupiter 8. Saturn 9.
Uranus 10. Neptune 11. Pluto 12. Nibiru.
IMANI NYINGINE YASEMA
MWISHO WA DUNIA NI FEBRUARI 22, 2014
Hata hivyo, utabiri mpya uliotolewa na watu wa jamii ya Vikings jijini New
York, Marekani umesema mwisho wa dunia ni Februari 22, mwaka huu.
Mitandao mbalimbali pamoja
na gazeti maarufu la Daily Mail la Uingereza lilielezea utabiri huo uliofanywa
na jamii hiyo ukidai kuwa mwisho wa dunia utatokana na Mungu Odin kupigana na
kuuawa na shetani Wolf Fenrir, hivyo kuiachia dunia anayoishikilia.
Wamesema baada ya kuiachia
dunia itafurika maji ambayo yatakuwa na sumu, hivyo viumbe wote watateketea.
WATUMISHI WA MUNGU TANZANIA
Baadhi ya watumishi wa Mungu nchini wamekuwa wakisimamia andiko la kwenye
Biblia linalosema kuwa, hakuna mwanadamu anayeijua siku wala tarehe ya mwisho
wa dunia na ni siri ya Muumba.
Makanisa mengi nchini
Tanzania yana sera tofauti lakini yanaongozwa na Biblia moja. Makanisa hayo ni
Romani Katoliki, Lutheran (KKKT), Anglikana na makanisa ya kiroho kama Full
Gospel& Bible Fellowship la Zakaria Kakobe.
FREEMASON WABARIKI
Jamii ya Freemason tayari imebariki mwisho wa dunia kwamba umefika na dunia
inatarajie tukio kubwa la pamoja.
Mitandao ya jamii hiyo
inataja kama hizi ni nyakati za mavuno kwa maana kwamba, upande wa Mungu na
shetani kushindania watu huku waendao upotevuni wakiwa wengi.
MFUMO WA DUNIA TANGU
KUUMBWA
Kwa mujibu wa kitabu kinachoitwa Panorama ya Biblia, ulimwengu tangu kuumbwa
kwake umekuwa na matukio makubwa kila baada ya miaka 2000 (inaweza isitimie au
ikapita kidogo).
Tangu kuumbwa kwa Adamu na
Eva mpaka gharika inadaiwa ni miaka 2000. Gharika hadi dunia kubadili mfumo wa
mawasiliano (Mnara wa Babeli) ni miaka 2000. Kuzaliwa kwa Yesu hadi saa ni
miaka 2000 ambapo katika karne hii, dunia huenda ikaingia katika tukio kubwa
sana ambalo halijawahi kutokea.
0 comments:
Post a Comment