Mzee
Philip Mangula Makamu Mwenyekiti wa CCM Bara akimkumbatia mgombea
ubunge wa jimbo la Kalenga kupitia Chama cha Mapinduzi Bw. Godfrey
Mgimwa kwenye eneo la Tosamaganga kata ya Kalenga mahali ambapo mkutano
wa hadhara wa kampeni umefanyika leo ikiwa ni mfurulizo wa mikutano hiyo
iliyofanyika katika vitongoji na vijiji vya kata ya Kalenga. Uchaguzi
wa jimbo la Kalenga unatarajiwa kufanyika Machi 16 jumapili ijayo ambapo
Mzee Philip Mangula amewaomba wananchi wa Kalenga kumchagua Godfrey
Mgimwa wa CCM kwa kura nyingi za ndiyo.

Sister
Paula Msambwa miaka 75 ambaye pia ni muuguzi katika hospitali teule ya
Tosamaganga na mwalimu wa Marehemu Dr.William Mgimwa aliyekuwa mbunge wa
jimbo hilo akitoa ushuhuda wake na kufurahia kumuona mjukuu wake
Godfrey Mgimwa akigombea ubunge katika jimbo la Kalenga Sister Paula
amekiri na kusema Marehemu Dr.William Mgimwa alipenda sana somo la
hesabu na alikuwa ni mwanafunzi mwenye kipaji na nidhamu

Sister
Paula Msambwa miaka 75 ambaye pia ni muuguzi katika hospitali teule ya
Tosamaganga akimuonyesha mgombea ubunge wa jimbo la Kalenga Bw. Godfrey
Mgimwa na kusema nimefurahi sana kuona mjukuu wangu akigombea ubunge.

Mwenyekiti
wa CCM Iringa vijijini Bi. Delfina Mtavilalu kushoto na Mwenyekiti wa
CCM mkoa wa Iringa Bi. Jesca Msambatavangu wakipiga magoti kumuombe kura
za ndiyo Bw. Godfrey Mgimwa katika kijiji cha Tosamaganga.

Mgombea
ubunge wa jimbo la Kalenga Bw. Godfrey Mgimwa akipokelewa kwa nderema
na vifijo mara baada ya kuwasili katika mji wa Kalenga mahali ambapo
amefanya mkutano wa hadhara leo na kuomba kura za ndiyo kwa wananchi.

Mgombea
ubunge wa jimbo la Kalenga Bw. Godfrey Mgimwa akibebwa juujuu mara
baada ya kuwasili Kalenga leo tayari kwa kufanya mkutano wa kampeni.

Wananchi
wakimpokea mgombea ubunge wa jimbo la Kalenga kwa tiketi ya CCM Bw.
Godfrey Mgimwa kwa picha zake mara baada ya kuwasili katika kitongoji
cha Ipamba kata ya Kalenga leo.

Msanii Dokii akiimba pamoja na wananchi katika kitongoji cha Ipamba kata ya Kalenga leo.

Akina mama wakionyesha picha za Bw. Godfrey Mgimwa kama ishara ya kumkubali.

Mgombea
ubunge wa jimbo la Kalenga kwa tiketi ya CCM Bw. Godfrey Mgimwa
akisalimiana na Masister mbalimbali wa parokia ya Tosamaganga

Wananchi wakinyanyua mikono yao juu kama ishara ya kumkubali mgombea huyo wa CCM.

Chifu Abdull Mkwawa akizungumza katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika mji wa Kalenga leo.

Makamu
Mwenyekiti wa CCM Mzee Philip Mangula akiwaelekeza wananchi jinsi ya
kupiga kura siku ya jumapili machi 16 ambapo amewaomba wanakalenga kwa
ujumla kumchagua Bw. Godfrey Mgimwa wa
CCM.
0 comments:
Post a Comment