Hii
ni habari ambayo ililipotiwa na vyombo mbalimbali vya habari kuhusu
Abria aliyejichinja ambaye alikua msafiri wa kutoka Lindi kuelekea Dar
es salaam,na bus alilosafiri nalo ni mali ya kampuni ya Maning Nice.
Basi hilo lenye namba za usajili T574 CQD ambalo linafanya safari zake za Dar es salaam na Mtwara saa 6 mchana,millardayo imepata nafasi ya exclusive interview na Dereva la basi hilo anayeitwa Rashidi Mohamed ambaye alikuwepo kazini siku ya tukio.

‘Abiria wote walipoteremka dakika 3 yule jamaa akarudi tena ndani ya
basi utaratibu wangu watu wote wakishuka huwa nafunga milango ya gari
kwa rimoti mpaka watu wote wakimaliza kula tunaingia tena ndani ya basi
kwa pamoja kwa ajili ya usalama zaidi’
‘Jamaa alivyopanda nikashangaa huyu jamaa mbona amepanda kabla ya
watu kumaliza chakula nilivyoenda kumuangalia nikamkuta ana sime yuko
kwenye boneti yani eneo langu la kazi yaani nikiwa na maana sehemu ya
kitanda nikamkuta anajichoma kisu aina ya sime’


‘Nikaanza kupiga kelele watu wakajaa tukamuita Meneja wa hotel
akapiga simu polisi baada ya nusu saa wakaja polisi lakini walikuta
jamaa yuko hoi ameshalala chini na damu zimetapakaa kwenye gari’
‘Yule jamaa nilipata neno lake moja anaitwa Kulwa kwa sababu yule
ndugu yake alivyokuja akaanza kupiga kelele huku akiita ‘Kulwa kwanini
unajiua,kulwa kwanini unajiua’baada ya hivyo yule ndugu yake akaanza
kukimbia’
‘Tulimfukuza akarudi pale akaanza kusema kuwa huyu jamaa alikuwa
anafanya kazi Lindi hakuwa na cha kuzungumza pale,baada ya polisi kuja
wakamchukua jamaa wakamuweka chini ya ulinzi na Yule jamaa mwingine
tayari macho alikua kashaanza kugeuza geuza’
‘Sisi tuliendelea kusubiri kuanzia hiyo saa 9 Alasiri mpaka saa 11
jioni mkuu wa kituo wa Kilwa Masoko alivyokuja kunihoji,mwisho wa mchezo
Yule jamaa akapelekwa Kilwa Masoko,lakini siku ya pili wakati tunarudi
Mtwara tulipishana nae na gari ya polisi analetwa Muhimbili baada ya
Madaktari wa Kilwa Masoko kushindwa hilo zoezi’
‘Pale hakufariki watu wote tuliamini amefariki maana macho
alishafumba na alikua hana uwezo maana hatua ya mwisho wakati anataka
kudondoka chini aliomba karatasi na kuandika ‘kaka’ halafu akakata kauli
hakuweza kuandika tena lakini aliashiria tumkamate yule jamaa yake
aliesafiri nae alikua akiashiria kwa mikono yake’
‘Humu ndani tulipakia wamasai 3 wale wamasai nahisi walivyoteremka
pale Nangulukuru kula mmojawapo alikua na Sime ambayo aliiacha kwenye
kiti,walikua wamekaa siti namba 6 na 9 ni karibu na mbele hapa,nafikiri
walipoteremka jamaa aliliona lile sime na ndiyo maana wao walivyoteremka
tu kwenda kwenye chakula yeye akarudi kwenye basi’
‘Nafikiri alilidhamiria lile sime ndiyo maana alivyoingia tu alifanya
kile kitendo bila kuchelewa na wale wamasai baada ya kuja polisi
wakakataa lakini wawili walikua na mapanga yao kiunoni lakini yule mmoja
akakataa akasema ameliacha pale alisafiri na rungu tu’.
0 comments:
Post a Comment