Mzee wa kanisa la kiroho (jina linahifadhiwa kwa sasa), aliyetajwa kwa jina la Luca Pesa, mkazi wa Segerea, Dar, ameaibika baada ya kukurupushwa kwenye nyumba ya kulala wageni (gesti) akidaiwa kutaka kuvunja amri ya sita na binti ambaye ni msanii chipukizi wa filamu za Kibongo, Debora Jacob.
Tukio
hilo ambalo kamwe Luca hawezi kulisahahu maishani mwake, lilijiri
kwenye gesti hiyo iliyopo karibu na Kituo Kikuu cha
Mabasi cha Segerea,
Dar, Jumanne iliyopita huku mzee huyo akishushiwa tuhuma nzito ya rushwa
ya ngono kwa vibinti chini ya miaka 18.
Katika
tukio hilo, mzee huyo wa kanisa na msanii huyo wa Kundi la Maigizo la
Vivif lenye maskani yake maeneo hayo walikuwa wamejichimbia kwenye gesti
hiyo katika chumba ambacho mlangoni kilikuwa kimeandikwa Rombo kabla ya
kuchomolewa na kufikishwa kanisani kisha polisi.
Fumanizi
hilo lilikuwa limesukwa na wasanii wa kundi hilo kwa lengo la
kumkomoa mzee huyo wa kanisa ambaye alikuwa ni mfadhili wa kundi
lao aliyeanza kutumia mgongo wa ufadhili kuwatongoza mabinti
wa kundi hilo mmoja baada ya mwingine.
Wakiwa
ndani ya gesti hiyo, wasanii wa kundi hilo walivamia chumba
hicho na kuanza kumchomoa mzee huyo ambaye aliruka ukuta na
kudondokea kwenye matuta ya viazi.
mzee huyo ambaye aliruka ukuta na kudondokea kwenye matuta ya viazi.
Akiwa
anajizoazoa kwenye matuta hayo, kundi la wasanii hao lilimuunganishia
ambapo kabla ya kumnasa aliingia kwenye chumba cha nyumba iliyopo jirani
na gesti hiyo ili kujisalimisha.
Hata
hivyo, zoezi lake lilifeli baada ya wasanii hao kumtahadhalisha mwenye
nyumba hiyo kuwa wanamtaka mtuhumiwa wao la sivyo wangeichoma moto.
Baada
ya kuzingirwa na wasanii hao huku akihatarisha maisha yake kwa kuwa
wasanii hao walikuwa na hasira, aliona yasiwe makuu akaamua kuwaruhusu
wamtoe mtuhumiwa wao wakamalizane naye kanisani.
Alipotiwa
mikononi, mzee huyo wa kanisa aliomba apelekwe kanisani ambapo hapakuwa
mbali na eneo la tukio ili akahifadhi vitu vyake muhimu pamoja na
kuomba ushauri.
Kundi
hilo la wasanii lilimpeleka kanisani msobemsobe ambapo baada ya hatua
kadhaa polisi walitokea na kuwadhibiti wananchi wenye hasira na wasanii
waliotaka kumdhuru mzee huyo wa kanisa wakati akipelekwa kanisani.
Wakiwa
mitaani, njiani mabinti walikuwa wakipiga kelele ‘weraaa…ukomeee…’ huku
wakifurahia kufunga mitaa kwa madai kwamba mzee huyo wa kanisa alizidi.
Katika sekeseke hilo, polisi hao walimtia pingu mzee huyo wa kanisa na kuongoza safari ya kuelekea kanisani.
Wakiwa
kanisani hapo polisi walijitambulisha na kuwauliza wachungaji pamoja na
waumini wa kanisa hilo kama walimfahamu mzee huyo wa kanisa.
Kundi
la wazee pamoja na vijana wa kanisa hilo walikiri kuwa Luca ni mmoja wa
wazee wa kanisa hilo ndipo polisi hao wakamruhusu kuwakabidhi baadhi ya
vitu vyake ikiwemo simu na fedha kisha breki ya kwanza ikawa Kituo cha
Polisi cha Tabata-Shule ambapo alifunguliwa jalada la kesi namba
RB/3843/2014 -RUSHWA YA NGONO, KUWAWEKA KAMBI KINYUME CHA SHERIA WASICHANA WENYE UMRI CHINI YA MIAKA 18 NA KUWADHALILISHA KIJINSIA.
0 comments:
Post a Comment