Friday, July 11, 2014

6:52 AM

 
Mtangazaji maarufu nchini VJ Penny ambaye alikuwa mpenzi wa Diamond Platnumz amechumbiwa.  Kupitia Instagram Penny ameweka picha akiwa amevaa pete ya uchumba  na  kuandika  ujumbe  huu: “Road trip

….site her we come…cc @halimakimwana1.” 
 
Pia juzi  tulisikia   kuwa Penny amechumbiwa ingawa hatukupata habari kwa kina mpaka Penny mwenyewe alipoweka picha Instagram  akiwa  amevaa  pete  ya  Uchumba.
VJ Penny ambaye  inadaiwa alikuwa chaguo la kwanza la mama Diamond Platinumz ameweka picha hiyo siku moja baada ya Wema Sepetu kupost picha nyingi kwenye Instagram akiwa na mama Diamond kwenye sherehe ya siku yake ya kuzaliwa na kuzipa caption mbalimbali huku nyingine zikiwa na vijembe

0 comments:

Post a Comment